1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Jake Sullivan akutana na Wang Yi mjini Beijing, China

27 Agosti 2024

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani Jake Sullivan anafanya ziara ya siku tatu nchini China na leo amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi mjini Beijing.

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani Jake Sullivan (kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi mjini Beijing ( kulia) kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing mnamo Agosti 27,2024
Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani Jake Sullivan (kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi mjini Beijing ( kulia)Picha: Ng Han Guan/AP Photo/picture alliance

Walipokutana leo mjini Beijing, Sullivan na Wang Yi walisema kwamba wanatarajia kufanya mazungumzo yenye tija.

Sullivan amesema anasubiria mikutano kati yake na Wang ambapo wataangazia masuala wanayokubaliana na pia ambayo bado kuna tofauti ambazo wanatakiwa kushughulikia kwa umakini na kwa ufanisi.

Soma pia:China, Marekani kuzungumzia suala la Taiwan

Muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, Sullivan aliwaambia waandishi habari kwamba Rais Joe Biden amekuwa wazi katika mazungumzo yake na Rais Xi kwamba amejitolea kusimamia uhusiano huu muhimu kwa uwajibikaji.

Kwa upande wake, Wang amemwambiaSullivankwamba anatazamia mazungumzo yatakayokuwa na ufanisi wakati wa ziara ya afisa huyo wa Marekani tangu mwaka 2016.

Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na mwenzake wa Marekani Joe Biden (kulia)Picha: Doug Mills/AP Photo/picture alliance

Wang ameongeza kuwa anazitaka pande hizo mbili kusaidia mahusiano kati ya mataifa hayo ya China na Marekani kusonga mbele kuelekea maono ya San Francisco, akimaanisha mfumo uliowekwa na Marais Joe Biden na Xi Jinping wakati wa mazungumzo yao mjini humo mwaka jana.

Wang pia amesema uhusiano kati ya China na Marekani ni muhimu kwa nchi zote mbili na pia unaathiri ulimwengu mzima.

Sullivan anafanya ziara China kabla ya uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba

Sullivan na Wang wamekutana mara tano katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita huko Washington, Vienna, Malta na Bangkok, na pia pamoja na Biden na Xi katika mkutano wa kilele wa mwezi Novemba huko California.

Mikutano hiyo kati ya Wang na Sullivan wakati mwingine ilitangazwa tu baada ya kuhitimishwa na wawili hao kukaa pamoja faraghani kwa muda mrefu.

Ziara ya Sullivan pia inafanyika kabla ya uchaguzi wa Marekani wa mwezi Novemba.

Kabla ya ziara hiyo, afisa mmoja wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema Sullivan atajadili kuhusu Bahari ya China Kusini na wenzake mjini Beijing, pamoja na Wang.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW