1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamhuri ya Afrika ya Ufaransa yaikaripia Ufaransa

20 Oktoba 2021

Jamhuri ya Afrika Kati yaishambulia Ufaransa na kutuhumu waziri wake wa mambo ya nje kwa kuendeleza tabia ya kikoloni.

UN I Jean-Yves Le Drian
Picha: Luiz Rampelotto/EuropaNewswire/picture alliance

Hayo yanajiri kufuatia mvutano unaoendelea kuhusu uwepo wa wapiganaji wa Kirusi kwenye taifa hilo linaloandamwa na machafuko.

Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Sylvie Mbaipo-Temon amesema tabia ya Ufaransa ya kutaka kutawala maamuzi ya serikali mjini Bangui ni sharti ikomeshwe ikiwemo shinikizo lake la kupinga uwepo wa mamluki kutoka Urusi nchini humo.

Tamko hilo linafuatia madai yaliyotolewa na mwezake wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian aliyesema mamluki wa Urusi waliopelekwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kutuliza uasi ndiyo wanazidisha machafuko ikiwemo matendo ya kikatili.

Urusi  ilipeleka washauri wa kijeshi nchini humo tangu mwaka 2018 na baadae kutuma kundi la wapiganaji wa kampuni binafsi ya Wagner kuisaidia serikali hatua ambayo imeikasirisha Ufaransa, ambayo ni mkoloni wa zamani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW