1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Dominica

Jamhuri ya Dominica ´yakaza uzi´ mvutano wake na Haiti

18 Septemba 2023

Rais wa Jamhuri ya Dominica, Luis Abinader, ametetea uamuzi wake wa kuifunga mipaka na taifa la jirani la Haiti kufuatia mvutano juu ya ujenzi wa mfereji utakaochepusha maji ya mto unaokatisha kwenye nchi hizo mbili.

Ujenzi wa mfereji ukiendelea nchini Haiti
Ujenzi wa mfereji kwenye mto Massacre unatishia kuzitumbukiza Haiti na Jamhuri ya Dominica kwenye mvutano wa kutishaPicha: Ricardo Hernandez/AP Photo/picture alliance

Katika hotuba yake kwa taifa iliyorushwa moja kwa moja kupitia televisheni, kiongozi huyo amesema njia zote za anga, maji na nchi kavu zitaendelea kufungwa hadi ujenzi wa mfereji huo upande wa Haiti utakapositishwa.

Jamhuri ya Dominica ilitangaza kuifunga mipaka yake na Haiti siku ya Ijumaa kama hatua ya kupinga ujenzi wa mfereji huo wa kuchepusha maji ya mto Massacre unaolenga kuisaidia wilaya ya Haiti ya Maribaroux inayokabiliwa na ukame.

Akiituhumu Haiti kwa kukiuka mkataba baina ya nchi hizo mbili Rais Abinader amesema ujenzi wa mfereji huo utaharibu mazingira na kutishia ustawi wa wakulima wa Jamhuri ya Dominica.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW