1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya Uchaguzi, DRC kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi

31 Desemba 2023

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hii leo inatarajiwa kutangaza matokeo kamili ya awali ya uchaguzi wa urais uliofanyika Disemba 20.

DR Kongo Kinshasa 2023 | CENI-Hauptquartier
Picha: Saleh Mwanamilongo/DW

Upande wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unasema uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu na kutaka urudiwe.

Kulingana na tume hiyo, CENI, matokeo hayo ya urais yatatangazwa saa saba mchana kwa majira ya taifa hilo.

Idadi ya kura iliyotolewa na CENI wiki iliyopita ilionyesha Rais Felix Tshisekedi akiongoza dhidi ya wapinzani wake 18, wakati zaidi ya asilimia 72 ya kura karibu milioni 17.8 zikiwa zimehesabiwa hadi sasa.

Kundi la wagombea wa urais kutoka upinzani kwenye taarifa yao ya pamoja mapema leo limeitisha maandamano baada ya matokeo hayo ya awali kutangazwa  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW