1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC kuanza kutoa chanjo ya Malaria Jumanne

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Shirika la Afya Duniani WHO limesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, itaanza kampeni ya chanjo dhidi ya Malaria kuanzia Jumanne ijayo.

Picha ya ishara ya chanjo ya Malaria
Mhudumu wa afya akitayarisha chanjo ya malaria kwa mtoto katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Yala, Kenya, Oktoba 7, 2021.Picha: Brian Ongoro/AFP

Kwa mujibu wa shirika hilo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Wizara ya Afya ya nchi hiyo kutoa chanjo ya malaria. Chanjo za awali zitatolewa katika mkoa wa Kongo Kati, ulio Kusini Magharibi mwa nchi. Kulingana na WHO, awamu ya kwanza ya dozi zaidi ya laki sita ziliwasili mwezi Juni. Aina hiyo ya chanjo imeshatumika katika nchi nyingine za Afrika zikiwemo Kenya, Cameroon, Malawi na Benin. Ugonjwa wa Malaria unaoweza kusababisha kifo huambukizwa kwa binadamu kupitia mbu na miongoni mwa dalili zake ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa pamoja na homa ya manjano. Watoto wa umri wa chini ya miaka mitano ndio hufariki zaidi kwa Malaria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW