1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa DRC afanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri

24 Machi 2023

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamefanyika mabadiliko ya baraza la mawaziri usiku wa kuamkia leo.

Felix Tshisekedi | Präsident Demokratische Republik Kongo
Picha: Arsene Mpiana/AFP/Getty Images

Hatua hiyo imezusha maoni yanayotofatiana maoni miongoni mwa raia wa Kongo, na  hasa kuhusu kuteuliwa Vital Kamerhe kuwa naibu waziri mkuu anayehusika na uchumi na Jean-Pierre Bemba aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya naibu waziri mkuu mwenye dhamana ya ulinzi  wa kitaifa.

Wanasiasa hao wawili walitarajiwa kuwa wagombea urais kwenye uchaguzi unaopangwa kufanyika  mnamo Desemba mwaka huu. Baraza jipya la  watu 58, linamjumuisha pia Peter Kazadi  kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Tshisekedi. 

Soma pia: Tshisekedi amrejesha Jean-Pierre Bemba serikalini

Antipas Mbusa Nyamwisi pia ameteuliwa kuwa Waziri anayehusika na ushirikiano wa kikanda wakati ambapo mwanahabari mkongwe wa michezo Kabulo Mwana Kabulo amepewa wizara ya michezo.

Mabadiliko haya yamefanyika wakati Kongo ikibakiwa na miezi minane kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu na hivyo kuzusha maswali mengi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW