SiasaJamhuri ya Kongo
Jamhuri ya Kongo yajiandaa kwa uchaguzi wa Rais
13 Machi 2026
Matangazo
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82, na ambaye aliingia madarakani mwaka 1979, atachuana na wanasiasa wengine sita wasio na ushawishi baada ya vyama vikuu vya upinzani kuamua kutosimamisha wagombea.
Vigogo wawili wa upinzani Jean-Marie Michel Mokoko na André Okombi Salissa ambao inaaminika wangetoa changamoto kwa Rais N´Guesso wako gerezani kwa karibu muongo mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuhatarisha usalama wa taifa.
Licha ya utajiri mkubwa wa mafuta, Jamhuri ya Kongo inakabiliwa na mzigo wa madeni na uchumi unaodorora, huku viwango vya ukosefu wa ajira kwa vijana vimefikia asilimia 24.