Janga la njaa nchini Niger
25 Julai 2005Nchini Ujerumani mashirika mbalimbali ya kutoa misaada yanawaomba raia wa nchi hiyo kutoa michango. Lakini msaada huo utachelewa kuwafikia maelfu ya watu. Tatizo hili la njaa lilikuwepo kwa muda mrefu nchini Niger.
Kuna wanaouliza ni kwanini serikali ya nchi hiyo, pamoja na jumuiya ya kimataifa, walichukua muda kulitatua tatizo hili.
Watu wamekuwa wakifariki vijijini Niger kutokana na njaa kwa miezi kadhaa sasa. Hamna chombo cha habari kutoka nchi tajiri kilichopeleka wandishi wa habari wake kuripoti yanayotokea, kuonyesha picha za watoto wanaofariki, na kuamsha hisia za raia wa Marekani na Ulaya wasaidie.
Kwa mara nyingine tena linatokea janga la njaa nchini Niger, katika karne hi ya 21, janga ambalo wengi walisema hatutaliona tena, sababu dunia inaweza kulizuia lisitokee. Watu milioni 2.5 wako hatarini kutokana na njaa, wakiwemo watoto 150,000.
Ilikuwa wazi kwamba janga hili litatokea Niger. Takriban mwaka moja uliopita Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa lilitoa onyo juu ya uwezekano wa janga la njaa kutokea, lakini hamna aliyefuatilia.
Dunia ilikuwa inashughulika na masuala mengine, kama janga la Tsunami, lililotokea kwenye bara la Asia. Hata serikali ya Niger, yenye makao makuu kwenye mji mkuu wa Niamey, haikulipa suala la njaa kipaumbele. Janga hili la njaa ni la kubwa kuliko yote, katika kipindi cha miaka ishirini, na uwezekano wa kulizuia ulikuwepo.
Kwa muda mrefu tatizo la ukame lilikuwa linajulikana katika nchi zote za jirani.Matatizo makubwa yatatokea nchini Niger na katiika nchi za jirani, zilizo kwenye eneo la Sahel. Ukweli wa mambo ni kwamba nchi za Magharibi hazishiriki ipasavyo kutatua matatizo duniani, kama raia wake hawahusiki kwenye tatizo hilo.
Ni baada ya vyombo vya habari kuonyehsa picha za wanaokufa, ndio jumuiya ya kimataifa imeanza kushughulika.
Kundi la nchi nane tajiri duniani lilifikia makubaliano ya kusamehe madeni ya baadhi ya nchi masikini, ikiwemo Niger. Maonyesho ya muziki ya Live 8, yaliofanyika duniani kote, kwa ajili ya Afrika yalionyesha picha nzuri tu za bara hilo. Hamna aliyeulizia juu ya njaa nchini Niger.
Tangu miaka ya 90 idadi ya watu wanaoishi na tatizo la njaa imepanda hadi kufikia karibu milioni 60. Watu milioni 852 wanakuwa na tatizo la njaa kila mwaka. Katika waafirka watatu, moja ana lishe duni. Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa linahangaika kutafuta misaada kwa kupambana na tatizo hili.
Shirika hili halijapewa hata asilimia 20 ya fedha za kupambana na matatizo ya nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, kutoka kwa wanachama wa Umoja huo.
Mwanzo wa mwezi wa Julai shirika hilo lilikuwa linasubiria milioni 11 za dola za kimarekani, zilizoahidiwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Niger na Mali.
Watu wengi nchini Niger, na katika nchi za jirani, wanauliza nchi zao kusamehewa madeni inawasaidia nini kama wakati huu wa janga kama hili hawapewi msaada?
Inaelekea tatizo hili ni kubwa kuliko mtu anavyodhania mara ya kwanza, na vigogo wa nchi hiyo wanachangia. Kwa nini hawalipi janga hili kipaumbele? Wakati umefika kwa serikali hiyo kushughulikia majukumu yao, sababu kuwepo kwa njaa ni wazi kwamba wameshindwa kazi.
Lakini pia njaa ni tatizo ambalo linaweza kutokea kutonaka na matukio mengi. Mfano unaonekana huko Niger ambako watu wengi wanategemea kilimo. Mazao makuu ni karanga na pamba, ambayo kwa sasa hayauziki kwa wingi katika soko la kimataifa, kwa sababu hawawezi kushindana na bidhaa kutoka nchi zilizoendelea.
Bidhaa ambazo hutengenezwa kutokana na mazao ya wakulima wa nchi tajiri wanaopewa ruzuku na serikali zao.