Japan kuanza tena kulifadhili shirika la UNRWA
29 Machi 2024Matangazo
Japan ambayo ni mfadhili mkubwa wa sita kwa shirika hilo, iliungana na mataifa mengine kusimamisha kwa muda msaada wake kwa UNRWA, baada ya Israel kudai kuwa wafanyakazi 12 kati ya 13,000 wa shirika hilo, walihusika katika shambulizi la Oktoba 7 kusini mwa Israel lililofanywa na wanamgambo wa Hamas.
UN: Nusu ya wakaazi wa Gaza wanakabiliwa na baa la njaa
Awali waziri wa mambo ya nchi za nje wa Japan Yoko Kamikawa alikutana na mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini mjini Tokyo kujadili hatua zilizochukuliwa na shirika hilo kuimarisha utawala bora na uwazi.
Japan imesema ufadhili huo uliosimamishwa mwezi Januari utaanzishwa tena mwezi Aprili. Australia, Canada, na Sweden pia zilitangaza mwezi huu kuanza tena kulifadhili shirika la UNRWA.