1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Japan, Marekani kujadiliana masuala ya usalama

6 Januari 2023

Japan na Marekani zitafanya mkutano kuhusu usalama kati ya mawaziri wa kigeni na ulinzi mjini Washington, siku moja kabla ya Waziri Mkuu Fumio Kishida kuwasili katika mji mkuu wa Marekani wiki ijayo.

Japan USA | Fumio Kishida und Joe Biden
Picha: Japanese PM Press Office/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Ziara ya Marekani itakamilisha ziara ya Kishida katika kundi la nchi saba zilizoendelea zaidi kiviwanda, G7, huku Japan ikijitanua kijeshi na kuimarisha uhusiano wake na Marekani, wakati ambapo ushawishi wa China unaongezeka.

Kishinda ataanza ziara yake Jumatatu ijayo nchini Ufaransa, Italia, Uingereza na Canada kabla ya mkutano wa kilele na Rais Joe Biden, Januari 13.

Waziri wa ulinzi wa Japan Yasukazu Hamada na Waziri wa Mambo ya Nje Yoshimasa Hayashi watakwenda Washington kukutana na wenzao wa Marekani Lloyd Austin na Antony Blinken kwa mazungumzo ya usalama Jumatano ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW