SiasaJapan
Japan na China zakubaliana kufanya mazungumzo ya usalama
25 Desemba 2024Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Japan Takeshi Iwaya, ameyasema hayo kwa waandishi habari mjini Beijing baada ya kukutana na waziri mwenzake wa China Wang Yi. Katika ziara yake ya kwanza nchini China tangu kushika wadhifa wa waziri wa mambo ya nje wa Japan mapema mwaka huu, Iwaya amewambia Wang kwamba Japan inafuatilia kwa ukaribu hali ya Taiwan na nyendo za kijeshi za hivi karibuni. Hapo awali, Iwaya alikutana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang na kukubaliana kufanya kazi ili kujenga uhusiano chanya na wa utulivu. China na Japan ni washirika wakuu wa kibiashara, lakini kuongezeka kwa msuguano juu ya maeneo yanayozozaniwa na matumizi ya kijeshi kumedhohofisha uhusiano wao katika miaka ya hivi karibuni.