1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan yafanikiwa kurusha roketi jipya anga ya mbali

Sylvia Mwehozi
17 Februari 2024

Shirika la anga za juu la Japan JAXA, limetangaza kurusha kwa mafanikio roketi lake jipya leo Jumamosi, ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuchelewa kwa miaka mingi na kushindwa mara mbili.

Japan
Japan ikirusha roketi jipya la H3 anga ya mbaliPicha: Kyodo News/AP/picture alliance

Shirika la anga za juu la Japan JAXA, limetangaza kurusha kwa mafanikio roketi lake jipya leo Jumamosi, ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuchelewa kwa miaka mingi na kushindwa mara mbili. Shirika la anga limelitaja roketi hilo kwa jina la H3 na kusema kwamba limefanikiwa kuruka kama ilivyopangwa na kufikia Obiti.

Soma: NASA yarusha satelaiti za kuchunguza vimbunga vya kitropiki

Likiwa limetengenezwa na shirika la anga la Japan na kampuni ya Mitsubishi, roketi hilo limeundwa mahususi kwa ajili ya kubeba vifaa kwenye kituo cha kimataifa ya anga za juu, pia lina uwezo wa kubeba satelaiti ndogo mbili.

Mafanikio hayo ni msukumo mkubwa kwa programu ya anga za juu ya Japan wakati nchi hiyo, ikijaribu kubaki katika ushindani kwenye sekta ya anga za juu ulimwenguni.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW