Japan yafuta mpango wake wa kuzisaka na kuziua nyangumi
21 Desemba 2007Matangazo
TOKYO:
Japan imefuta mpango wake wa kuua nyangumi kufuatia malalamiko kutoka nchi za magharibi zikiongozwa na Australia.Japan ilikuwa imepanga kuwavua nyangumi 50 kwa kutumia mikuki katika safari mpya ya kuwasaka nyangumi katika ncha ya kusini ya dunia ya Antarctic.Safari hii ndio ya kwanza kufanywa na Japan tangu miaka ya 1960.Tomohiko Taniguchi ni afisa wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Japan.
Hata hivyo Japan inaendelea na safari yake katika maeneo ya Antarctic yenye lengo la kuwauwa nyangumi wapatao 1,000 wengi ni wa sampuli nyingine.Japan inasema hatua yake hii ni ya kitafiti.