1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Japan yaidhinisha bajeti ya ulinzi ya dola bilioni 56

23 Desemba 2023

Serikali ya Japan imeidhinisha bajeti ya ulinzi inayovunja rekodi kwa mwaka ujao. Matumizi ya kijeshi yataongezeka kwa asilimia 17 ikilinganishwa na mwaka wa sasa wa kifedha hadi dola bilioni 55

Japanische Luftselbstverteidigungskräfte
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alitangaza kuongeza bajeti ya JapanPicha: Yoshio Tsunoda/AFLO/IMAGO

Serikali ya Japan imeidhinisha bajeti ya ulinzi inayovunja rekodi kwa mwaka ujao. Matumizi ya kijeshi yataongezeka kwa asilimia 17 ikilinganishwa na mwaka wa sasa wa kifedha hadi dola bilioni 55.

Soma pia: Marekani, Korea Kusini, Japan kukutaka kwa kujadili usalama

Mipango ya Japan kulipa jeshi lake silaha nyingi kimsingi inalenga kupambana na kujitanua kwa China na mpango wa silaha za nyuklia na makombora wa Korea Kaskazini, ambao Tokyo inauona kama kitisho.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alikuwa ametangaza mipango ya kuongeza bajeti ya Japan hadi asilimia mbili ya Pato Jumla la Ndani. Fedha zilizoongezwa zitatumika kuharakisha manunuzi ya makombora ya masafa marefu.

Aidha, bajeti hiyo italiongeza nguvu jeshi lake kwa kununua ndege za kivita aina ya F-35 na zana nyingine za Marekani.