1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan yamuachia mfungwa aliyetumikia adhabu ya kifo

Josephat Charo
26 Septemba 2024

Bondia wa zamani wa Japan aliyetiwa hatiani miaka zaidi ya 50 iliyopita kwa kumuua bosi wake pamoja na familia yake amefutiwa makosa na mahakama ya Japan hivi leo.

Iwao Hakamada
Iwao HakamadaPicha: Kyodo News/AP/picture alliance

Bondia wa zamani wa Japan aliyetiwa hatiani miaka zaidi ya 50 iliyopita kwa kumuua bosi wake pamoja na familia yake amefutiwa makosa na mahakama ya Japan hivi leo.

Mahakama ya wilaya ya Shizuoka imepitisha hukumu kwamba Iwao Hakamada mwenye umri wa miaka 88 hakuwa na hatia, katika kesi iliyosikilizwa upya, iliyoruhusiwa miaka 10 iliyopita.

Soma: Waziri Mkuu wa Japan Kishida hatagombea tena uenyekiti wa chama chake

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Japan NHK, jaji aliyesimamia kesi hiyo, Koshi Kunii, amesema mahakama imekubali kulifanyika upotoshaji mwingi wa ushahidi na kwamba Hakamada siye aliyefanya mauaji hayo.

Hakamada ni mfungwa wa tano aliyekabiliwa na hukumu ya kifo kuruhusiwa kesi yake isikilizwe upya katika historia ya Japan baada ya kumalizika vita. Kesi nne za awali pia zilikamilika kwa wafungwa kufutiwa makosa na kuachiwa huru.