1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan yatishia kupunguza michango yake ya fedha

28 Julai 2005

New York:

Japan imetishia kuwa itapunguza michango yake ya fedha ya Umoja wa Mataifa ikiwa haitafanikiwa kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Japan, Nobutaka Machimura, amesema mjini New York kuwa ikiwa nchi yake haitakuwa na kiti cha kudumu, kutakuwa na shinikizo kubwa ndani ya Japan la kutaka michango yake ya fedha ipunguzwe. Japan baada ya Marekani inatoa michango mikubwa katika Umoja wa Mataifa. Serikali ya Japan mwaka uliopita imegharimia asili mia 20 ya bajeti yote ya Umoja wa Mataifa. Balozi wa Italia kwenye Umoja wa Mataifa, Marcello Spatafora, jana amesema kuwa Ujerumani, Japan, India na Brazil, kikundi kinachojulikana kama G4, zimetishia kuwa iwapo hazitaungwa mkono na nchi za Kiafrika katika juhudi zao za kupata viti vinne vya kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zitapunguza misaada yao kwa nchi zinazohusika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW