Jaribio la mapinduzi linaendelea nchini Niger
26 Julai 2023Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya zimelaani kile zilichokiita jaribio la Mapinduzi, maelezo ambayo yametumiwa pia na chanzo kilichoko karibu na Bazoum, kikibashiri kuwa jaribio hilo litafeli. Kikosi cha ulinzi wa rais leo asubuhi kilizuwia njia ya kuingia kwenye makazi ya rais na ofisi yake, na baada ya mazungumzo kushindikana, walikataa kumuachia rais, kimesema chanzo kingine.
Jeshi lasema liko tayari kushambulia
Chanzo hicho kimesema jeshi limewapa wanajeshi hao muda, na kusema liko tayari kuwashambulia ikiwa hawatatii. Bazoum ambaye ni mshirika wa karibu wa Ufaransa, alichaguliwa mwaka 2022, na kuchukua mamlaka katika taifa hilo linalokabiliwa na umaskini mkubwa na lenye historia ya kukosa utulivu.