1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jasusi wa Urusi akamatwa nchini Ujerumani

11 Agosti 2021

Waendesha mashitaka, Ujerumani wamesema wanamzuilia raia mmoja wa Uingereza anayetuhumiwa kufanya ujasusi kwa niaba ya Urusi wakati anafanya kazi katika ubalozi wa Uingereza mjini Berlin Ujerumani.

Berlin Botschaft Großbritannien Wilhelmstrasse
Picha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Katika taarifa iliyotolewa leo na waendesha mashitaka nchini Ujerumani wamesema mtu huyo alikamatwa jana Jumanne katika mji wa Postdam baada ya uchunguzi wa pamoja kati ya maafisa wa Ujerumani na wa Uingereza.

Ili kuzingatia sheria ya faragha ya Ujerumani mwanamume huyo ametambulika kwa  David S. Inaarifiwa kwamba amekuwa akifanya upelelezi kwa niaba ya shirika la ujasusi la Urusi tangu mwezi Novemba 2020. Soma Maafisa wa zamani wa ujasusi wa Syria kushitakiwa Ujerumani

Kabla ya kukamatwa kwake, mshukiwa huyo aliajiriwa kama mfanyakazi mwenyeji katika Ubalozi wa Uingereza katika mji mkuu wa Ujerumani na inadaiwa alilipatia shirika la kijasusi la Urusi, FSB nyaraka za ubalozi wa Uingereza kuhusu mkakati dhidi ya ugaidi.

Ujerumani inaifuatilia keshi hio

Vladimir Putin rais wa UrusiPicha: Yevgeny Odinokov/TASS/dpa/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Ujerumani Christofer Burger amesema serikali inaifuatilia kwa karibu kesi hiyo.

"Tunachukulia madai kwamba shughuli za ujasusi ya mtu aliyekamatwa zilifanywa kwa niaba ya huduma ya ujasusi ya Urusi kwa umakini sana. Huduma ya siri kupeleleza mshirika wa karibu kwenye ardhi ya Ujerumani sio jambo ambalo tunaweza kukubali, ndiyo sababu tutafuata uchunguzi zaidi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa karibu sana."

Hata hivyo  Urusi bado haijatoa kauli yoyote kuhusu madai ya kuhusika. soma Urusi yazidi kubanwa mgogoro wa sumu dhidi ya jasusi

Mshukiwa alipokea pesa taslim

Polisi ya Uingereza katika taarifa tofauti imesema kuwa mtu huyo alikamatwa mjini Berlin  kwa tuhuma za makosa yanayohusiana na kushiriki katika shughuli ya Uwakala wa Ujasusi.

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamesema mshukiwa alipokea kiasi kisichojulikana cha pesa taslimu kwa malipo ya shughuli zake za ujasusi. Wachunguzi walifanya upekuzi nyumbani na ofisini kwa mshukiwa huyo.

Mshtakiwa atafikishwa mbele ya jaji anayechunguza kesi hio katika korti ya shirikisho, ambaye atamsomea mashtaka na kuamua ikiwa utamuweka rumande.

Katika miaka ya hivi karubuni Ujerumani imewakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kwa ujasusi kwa niaba ya Urusi, lakini kukamatwa kwa raia wa nchi mshirika wa karibu kama Uingereza ni hali isio ya kawaida.

 

Vyanzo: (Reuters) AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW