Java:kimbunga chauwa huko Indonesia.
17 Julai 2006Matangazo
Watu 20 wamekufa baada ya kimbunga kupiga majengo kadhaa kusini mwa ufukwe wa Indonesia katika kisiwa cha Java.
Tukio hili limekuja baada ya kuongezeka kwa tahadhari ya kutokea kwa Tsunami kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea leo nchini humo lenye ukubwa wa 7.2 kwa kipimo cha rishta.
Rais wa Indonesia Susilo Bambang Yundhoyono akizungumza na kituo cha radio nchini mwake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mnamo Desemba 2004 karibu watu 230,000 walifariki dunia na wengine zaidi ya 43,000 hawakujulikana walipo katika tetemeko la ardhi lililotokea Indonesia na janga la Tsunami lililoikumba bahari ya Hindi.