1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Je vizingiti vilivyomzuia Assad kukubalika vinapanguka?

Zainab Aziz Mhariri: Grace Patricia Kabogo
11 Januari 2023

Kauli zilizotolewa hivi karibuni na viongozi wa Uturuki na wa nchi za kiarabu zinaashiria uwezekano wa Rais Bashar al Assad na utawala wake kurejeshwa tena katika uhusiano wa kimataifa.

Syrien | Bashar Assad und Recep Tayyip Erdogan
Picha: SANA/AP/picture alliance

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Syria Bashar al-Assad wamekuwa hawapatani kwa miaka mingi, lakini sasa inaonehsa kuwa wanaweza wanaweza kurudisha uhusiano mwema kati yao. Hiki ndicho alichokionyesha rais wa Uturuki mwishoni mwa wiki iliyopita pale alipoashiria kuwa hakatai kukutana na Assad na kuhusu Syria, Erdogan aliuzungumzia mchakato mpya wa amani ambapo alisema Urusi, Uturuki na Syria zinashirikiana kwa pamoja.

Kushoto mbele: Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Kulia mbele: Rais wa Syria Bashar al-Assad.Picha: BULENT KILIC/AFP/Getty Images

Awali ulifanyika mkutano wa wakuu wa kijasusi na mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo tatu mjini Moscow na  kulingana na Erdogan, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu watakutana ambapo vyombo vya habari, vimeripoti kwamba mkutano huo unaweza kufanyika leo Jumatano.

Soma: UN yapitisha azimio kupeleka misaada Syria

Mkuu wa idara ya maswala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Wakfu wa Heinrich Böll: Bente Scheller amesema kwa hatua hizo rais wa Syria Bashar al Assad anatumai kuwa zitampa nguvu ya kidiplomasia. Amesema ingekuwa na thamani zaidi kwake ikiwa nchi za Ulaya au Marekani ndio zingetaka kurejesha uhusiano mzuri na Syria. Kwa hiyo rais wa Syria anatumai uhusiano kuimarika sio tu kati ya Syria na Mataifa ya Ghuba, lakini pia na Uturuki na Jordan kwa sababu serikali yake inahitaji pesa haraka kufadhili ujenzi mpya wa Syria lakini hadi sasa hakuna matarajio yoyote kutoka kwa nchi jirani au mataifa ya Ghuba yakiwekeza nchini Syria kwa namna yoyote.

Wadadisi tayari wanaiona hatari ya kurejea hatua kwa hatua kwa Assad katika ngazi ya kimataifa, huku wapinzani wa serikali ya Syria wanahisi kusalitiwa na Erdogan na wamekuwa wakipinga kwa sauti kubwa mpango huo wa kukaribiana viongozi hao wa Syria na Uturuki kwa muda mrefu.

Kushoto: Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Kulia: Rais wa Urusi Vladimir Putin.Picha: Mikhail Metzel/ITAR-TASS/IMAGO

Mkuu wa idara ya maswala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Wakfu wa Heinrich Böll, Bente Scheller anasema maoni yake juu ya marekebisho ya kisiasa yanayoendelea ambayo yanalenga rais Assad kubakishwa madarakani daima litakuwa janga la utamaduni wa kisiasa ndani na nje ya eneo la Mashariki ya Kati kwa sababu mengi ambayo Assad ameyapata yaliwezekana tu kutokana na ukiukaji mkubwa wa kanuni za kimataifa.

Amesema ni hatari iwapo wenye nguvu au wanaodhaniwa kuwa na nguvu zaidi watapewa nafasi bila kujali kukiuka kanuni, katiba, mikataba na sheria zote zinazotumika.