Je, DRC itafanikiwa ikiwa itaachana na dola?
15 Desemba 2023Wapiga kura wengi wanataka kuona matumizi ya dola yakitupiliwa mbali. Akiwa ameketi kwenye kiti kidogo katika soko maarufu la Lumumba, lililoko katika wilaya ya Bandalugwa katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasa, mfanyabiashara Rosette Kungi anachanganya maharage kwenye ndoo kubwa ya kijani karibu na alama zake za bei zinazobadilika kila siku.
Katika miezi ya hivi karibuni, sarafu ya Jamhuri ya Kidemokrasia, faranga ya Kongo (CDF), imeshuka thamani sana. Nikimnukuu hapa Kungi anasema "Bei ya faranga ya Kongo haitabiriki kila wakati."Leo, dola 10 inathamani ya 27,000, au hata faranga 28,000 na hivi karibuni itakuwa 30,000." Ameiambia DW kasha la samaki ambalo lilikuwa likiuzwa dola 15, kwa sasa limefikia dola 80.
Mabadiliko ya manununzi ya bei za bidhaa ya kila siku
Mfanyabiashara mwingine, Helene Timba, anasema anakabiliwa na mabadiliko ya bei kila siku. Huku akipipunga nzi waliotua kwenye kibanda chake cha samaki wabichi, alisema kuwa kupanda bei ya bidhaa umekuwa mjadala wa karibu kila uchao.
Nikimnukuu hapa anasema "Tunanunua gunia la maharage kwa dola, lakini tunauza kwa faranga za Kongo, na kama tunataka kununua zaidi, lazima tununue dola, jambo ambalo linafanya maisha yetu kuwa magumu."
Je, kuachana na matumizi ya dola nchini Kongo kunaweza kusaidia uchumi wake?
Kwa namana isiyo rasmi uchumi wa nchi hiyo ulikuwa wa "dola" katika miaka ya 1994, wakati DRC ilipojulikana kama Zaire na kuongozwa na kiongozi mbabe Mobutu Sese Seko. Mfumuko wa bei ulikuwa umefikia kiwango cha juu kabisa na kusababisha kuporomoka kwa uchumi. Dola ya Marekani bado inachukuliwa kuwa sarafu kuu ya kibiashara ya DRC, wakati mishahara inaendelea kulipwa kwa sarafu ya taifa.
Soma zaidi:Kuelekea kura DRC, vijana watamani ajira
Bidhaa nyingi za nchi hiyo zinaagizwa kutoka nje, na vita vya Ukraine vimesababisha bei ya ngano, mafuta na bidhaa nyingine kupanda. Watu milioni 60 wa Kongo wanaishi chini ya dola 2.15 kwa siku, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.
Chanzo: DW