1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, kuna mpasuko ndani ya Chadema?

9 Desemba 2024

Wakati Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA kikijiandaa na uchaguzi mkuu wa Taifa wa chama hicho, tayari zimeibuka taarifa za baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho kutaka kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Taifa.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema Freeman MbowePicha: Ericky Boniphace/DW

Wadhfa huo umekuwa ukishikiliwa na mwenyekiti wa sasa Freeman Aikael Mbowe kutoka mwaka 1995 huku taarifa hizo za baadhi ya wanachama kutaka kurithi mikoba ya Mbowe, zikitafisiriwa kama mpasuko ndani ya chama hicho na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na baadhi ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii.

Tundu Lissu Makamu mwenyekiti wa Chama hicho na mgombeaUrais wa Chadema kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 jina lake limekuwa likitajwa  huku yeye mwenyewe mpaka sasa akiwa hajatoa kauli rasmi ya kukubali kumkabili Mbowe kama shinikizo la baadhi ya wanachadema linavyovuma.

Kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu LissuPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Mbowe anatajwa kuwa mwanasiasa aliyeiongoza Chadema kwa mafanikio tangu ashike mikoba hiyo kutoka kwa Edwini Mtei ambaye pia anatajwa kukivusha Chadema wakati mgumu wa siasa za Tanzania.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii nchini Tanzania wanaona kama Lisu atajitokeza kupambana na Mbowe itakuwa ni kipimo sahihi cha Demokrasia ndani ya CHADEMA.

Viongozi watakaochaguliwa kuiongoza CHADEMA, jukumu lao la kwanza itakuwa ni kukivusha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu mwakani ambao CHADEMA watakuwa wanapambana kurudisha nguvu waliyokuwa nayo kabla ya mwaka 2015.

Mwandishi: Dotto Bulendu

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW