Je, michuano ya AFCON 2024 itakuwa ya ushindani zaidi?
10 Januari 2024Katika michuano 37, nchi 15 tofauti zimejishindia kombe hilo la AFCON.
Kimsingi kila taifa linalotambulika kwa umahiri wa soka barani Afrika limeshinda kombe hilo angalau mara moja na baadhi ya nchi ndogo pia zimeweza kushinda, kama vila Zambia mnamo mwaka 2012.
AFCON imekuwa ikipendelea timu kubwa katika miaka ya karibuni
Katika miaka ya hivi karibuni, AFCON imekuwa ikipendelea timu kubwa kama Algeria au Senegal, hata hivyo historia imeonyesha kuwa lolote linaweza kutokea wakati wa michuano hiyo.
Soma pia: Sadio Mane asema wako katika kundi gumu AFCON
Kama vile Didier Drogba, anavyochukuliwa na wengi kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa soka barani Afrika, hakuweza kushinda kombe hilo licha ya kuwa sehemu ya kile kinachoitwa kizazi cha dhahabu cha Ivory Coast,pamoja na wachezaji kama Yaya Toure na Gervinho, miongoni mwa wachezaji wengine tajika.
Sadio Mane asema michuano ya AFCON ya mwaka 2024 ni migumu kutabiri
Nyota wa Senegal Sadio Mane anasema kuwa michuano ya AFCON ya mwaka 2024 ni migumu zaidi kutabiri.
Pengine Mane anajaribu kupunguza shinikizo, kwa kuwa mabingwa watetezi wa AFCON Senegal ni mojawapo ya timu zinazosubiriwa sana mwaka huu, lakini hiyo haimaanishi kuwa hajishughulishi na matayarisho yoyote.
Soma pia;Victor Boniface kuikosa michuano ya AFCON kutokana na jeraha
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, Ivory Coast sio timu inayoonekana ikipigiwa upatu zaidi.
Ibrahim Traore, mchezaji wa zamani wa ligi ya Ujerumani Bundesliga, na pia nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Guinea, anasema Senegal, bila shaka, ni timu ya kutazamwa, kwa sababu ni timu ambayo inaweza isionekane kuwa ya kuvutia kama nyingine kwa soka, lakini ni timu ambayo imezoea kufika mbali kwenye mashindano na kufanya kile kinachohitajika ili kupata ushindi.
Soma pia:Wenyeji wa AFCON Ivory Coast wapangwa kundi moja na Nigeria
Mataifa mengine pia yana hoja za kuwasilisha.
Morocco itataka kuonyesha kwamba matokeo yao mazuri wakati wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 ambapo ilimaliza katika nafasi ya nne, hayakuwa bahati tu.
Soma pia:Kenya, Tanzania na Uganda zaomba kwa pamoja kuwa mwenyeji michuano ya AFCON 2027
Misri inaweza kutegemea kundi dhabiti la wachezaji kutoka Al Ahly na Zamalek, vilabu viwili vikubwa zaidi barani Afrika, na itajaribu kumjumuisha Mohamed Salah katika michuano yake ya kwanza ya AFCON .
Timu nyingine zinazoweza kujipatia ushindi
Timu nyingine zinazoonekana kuweza pia kujipatia ushindi kwenye michuano ya mwaka huu ya AFCON ni Cameroon, Ghana, Mali, Guinea, Burkina Faso, Tunisia na bila shaka mwenyeji Ivory Coast.
Soma pia: Mataifa ya Afrika Mashariki yaandika historia AFCON
Kwa kuwa mashindano haya hayana timu inayopendelewa kwa wazi, kuna wachezaji nyota wengi ambao watafanya kila kitu kusaidia timu zao kufikia malengo yao.
Soma pia:Tanzania yafuzu fainali ya michuano ya AFCON
Lakini hata kama wamecheza na kuishi nje ya nchi kwa miaka mingi na baadhi yao tayari wameshinda mataji kadhaa ya kifahari, kama vile Ligi ya Mabingwa, kushinda AFCON bado ni lengo lao kuu.