1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, mkimbizi atabaki tu kuwa mkimbizi?

26 Agosti 2016

Licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Ujerumani bado wapo wakimbizi wanaokabiliwa na matatizo kiasi cha kutaka kurejea katika nchi zao.Ni wakimbizi waliovunjika moyo.

Griechenland Flüchtlinge bei Idomeni
Picha: Getty Images/AFP/D. Dilkoff


Hayo yamemkuta Sally Abazid kutoka Syria. Baada ya kuwapo nchini Ujerumani kwa muda wa miezi tisa alihisi kuwa bado hajakaribishwa vizuri.

Mkimbizi huyo Sally Abazid alisema akiwa amekasirika kwamba hata baada ya kuwapo nchini Ujerumani kwa muda wa miezi kadhaa alikuwa bado hajapata kibali rasmi cha kumruhusu kuishi nchini. Kutokana na hali hiyo hakuweza kupata makaazi.

Katika wiki ya kwanza baada ya kuwasili nchini Ujerumani mama huyo aliwekwa kwenye sehemu ya kujishikiza, kwenye ukumbi wa michezo.Lakini kwa sababu yeye nimtu mwenye uhusiano wa kimapenzi na wanawake na wanuime alihamishiwa kwenye dahalia ya mashoga mjini Berlin.

Wakimbizi wanafunzi wakiwa darasani mjini Berlin.Picha: DW/K.Salameh

Lakini uamuzi huo ulimkasirisha. "Hapo nilipaswa kulala chumba kimoja na wavulana watatu. Hilo lilinichefua sana." Aliamua kwenda kuishi na marafiki zake kwingineko, lakini huo haukuwa uamuzi mzuri kwani wakati wote alipaswa kuhama.

Waondoka kwa hiari

Kwa mujibu wa idara ya Ujerumani inayowashughulikia wakimbizi na wahamiaji, BAMF mnamo nusu ya mwaka huu wakimbizi 35, 000 waliondoka nchini Ujerumani. Watu hao waliondoka kwa hiari, chini ya mpango unaodhamiwa na idara hiyo.

Idadi kubwa miongoni mwao walipitia njia ya Balkan, kusini mashariki mwa Ulaya, na hawakuwa na ruhusa ya kuingia nchini Ujerumani. Hata hivyo baadhi yao walikuwa tayari wameshatoa maombi ya hifadhi ya ukimbizi. Lakini baadae waliamua kwa hiari zao kuondoka Ujerumani na kurejea katika ncho zao au kwingineko.

Lakini mambo ya Sally ni tafauti kabisa. Yeye hana majonzi juu ya kuondoka Syria. Kwani hana mtoto wala mtu mwengine yeyote anaepswa kuwa pamoja naye. Hakuna mtu yeyote katika familia yake aliekufa kutokana na vita.

Sally Abazid anatoka mji wa Damascus. Anatoka tabaka la kati. Alisomea taaluma ya habari na mawasiliano kwenye chuo kikuu. Lakini mapema kabisa aliweza kutambua kwamba alikuwa anaishi katika mazingira ya kukatisha tamaa kutokana na vita vya nchini mwake.

"Nilikuwa bado naenda shule, wakati vita vilipoanza. Tayari wakati huo nilikuwa nawaza kukimbia. Nilipata matatizo kutokea ndani ya familia yangu kutokana na itikadi za kihafidhina za kidini."

Waomba hifadhi mjini BerlinPicha: Getty Images/S. Gallup

Sally Abazid hakuwa na uhuru wa kuchagua la kufanya katika maisha yake. Na kutokana na mwelekeo wake wa kijinsia - wa kufanya mapenzi na wanaume na wanawake wenzake, hakukubalika katika jamii ya kihafidhina.

Na kwa hivyo alibakiwa na njia moja tu, kuondoka Syria na kuanza maisha kwingineko. Aliamua kwenda Ulaya ambako amesema kuna uhuru na haki sawa. Ni kweli ameona pana usawa nchini Ujerumani, lakini ni miongoni mwa Wasyria na wakimbizi wenzake tu. Jee mkimbizi, daima ataendelea kuwa mkimbizi?

Mwandishi:Melhem, Maissun
Mfasiri:Mtullya Abdu
Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW