Je, ni Mourinho atakayeinoa Benfica?
17 Septemba 2025
Tangazo hilo limethibitishwa na klabu hiyo huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa miamba hao wa Ureno sasa wako katika mazungumzo na Jose Mourinho ambaye aliachishwa kazi na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce wiki chache zilizopita.
Benfica walishindwa 3-2 na Qarabag licha ya kuiongoza mechi hiyo ya ufunguzi wa ligi hiyo ya mabingwa 2-0.
Na sasa kama inavyodaiwa na vyombo vya habari, huenda Mourinho akarudi tena katika klabu hiyo baada ya kuanza taaluma yake hapo Benfica kabla kuondoka baada ya miezi miwili na nusu tu na kuelekea kujiunga na mahasimu wao FC Porto, alikojijengea jina.
"Tumekubaliana na Bruno Lage kwamba aiache nafasi yake kama kocha wa Benfica leo," alisema Rui Costa, rais wa Benfica.
Lage ambaye aliwahi kuifunza Wolverhampton Wanderers ya England, tayari alikuwa chini ya shinikizo kabla ya kipigo hicho cha Qarabag kwa kuwa alikuwa amepoteza pointi zake za kwanza katika ligi ya nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Santa Clara.