Jamii nyingi za kiafrika zilitumia njia za asili kusafisha meno na kinywa kama moja ya njia ya kulinda meno yasishambuliwe na magonjwa mbalimbali. Njia hizo zilihusishwa mishwaki iliyotokana na miti, kutumia chumvi, majivu na vitu vingine vya asili kwaajili ya kusafisha kinywa.