1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, uchaguzi wa Marekani unaweza kuamuliwa mahakamani?

6 Novemba 2020

Mwaka 2000, uchaguzi wa rais uliamuliwa mahakani - na mwaka huu unaweza kuketa mashaka sawa na hayo. Wakati kura zikiendelea kuhesabu, Donald Trump alijitangazia ushindi. Je, uchaguzi huu unaweza kuamuliwa mahakamani?

US Wahlen 2020 | Donald Trump Rede
Picha: Carlos Barria/Reuters

Wakati kura zikiendelea kuhesabiwa katika majimbo muhimu ya maamuzi, rais wa sasa Donald Trump tayari anajaribu kuunda simulizi. Akizungumza na wafuasi wake ikulu ya White Housemapema Jumatano asubuhi akidai kabla ya matokeo rasmi kwamba ameshinda uchaguzi huo.

Trump aliwaambia wafuasi wake wakati wa hotuba hiyo fupi kwamba kambi yake itapeleka madai yake mahakama ya juu. Haijulikani hasa ni suala gani rais huyo na timu yake wanapanga kupeleka mahakamani, ingawa katika ujumbe wake uliyofuatia, alisema wanataka kusitisha zoezi lote la kuhesabiwa kura.

Soma pia Biden aongoza katika majimbo muhimu, Georgia na Pennsylvania

Kwa ufafanuzi, kura zote zilikuwa zimepigwa, zikiwemo kura zilizotumwa kwa njia ya posta, wakati Trump alitopoa hotuba yake - na waangalizi wanasema yumkini alimaanisha kusitisha hesabu ya kura za raia waishio nje na zile za posta, ambazo zilionekana kumuongezea nguvu mshindani wake Joe Biden katika majimbo yenye ushawishi ya Michigan na Pennsylvania.

Joe Biden anaongoza dhidi ya rais Donald Trump.Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Matokeo ya mwisho huchukuwa muda kukamilika

Ni kawaida kwamba matokeo ya mwisho hayajulikani usiku wa uchaguzi,kama ailivyosema Kamishna wa tume ya uchaguzi ya shirikisho Ellen Weintraub,katika mazungumzo na kituo cha CNN. Alisema matokeo rasmi huja wiki kadhaa baadae. Kamishna huyo alisema jambo muhimu zaidi ni kwamba kura zote zinahesabiwa.

Wachambuzi wa DW wanasema kuna muda wa kutosha tu kuhesabu kura zote zilizopigwa kihalali: Majimbo 21 yanakubali kura zinazowasili baada ya siku ya uchaguzi ili mradi tu zimeainishwa, katika kesi hii, Novemba 3, na kupokelewa na maafisa wa uchaguzi kufikia tarehe makshusi.

Soma pia Biden apata kura zaidi Georgia na kumpiku Trump

Miongoni mwa majimbo hayo ni Pennsylvania, Nevada na North Carolina - ingawa muda wa mwisho wa kukubaliwa kwa kura unatofautiana kati ya jimbo na jimbo.

Wafuasi wa Trump waandamana Biden akiongoza uchaguzi

01:01

This browser does not support the video element.

Mawakili wajiweka tayari kwa mapambano

Hii inarudisha kumbukumbu ya uchaguzi wa mwaka 2000, wakati jimbo muhimu la Florida lilipogeuka kivutio cha nadharia ya kitaifa.

Hesabu za awali zilionesha mgombea wa Democratic, makamu wa rais Al Gore akiwa nyuma ya mrepublican George W. Bush kwa kura 1,800 tu. Katika mgawanyo wa kura ya wajumbe maalumu, Florida, kama yalivyo majimbo mengi, inatumia kanuni inayotoa kura zote kwa mshindi wa kura ya raia.

Soma piaNini kitatokea kama matokeo ya uchaguzi wa Marekani yatapingwa? 

Wakati Bush na Gore wakiwa wamefungana, maafisa wa uchaguzi jimboni Florida walishikilia funguo za White House.

Gore ambaye alikuwa tayari amempigia Bush simu kumpongeza juu ya ushindi wake, alitoa wito wa kuhesabiwa upya kwa kura jimboni Florida - jambo linaloruhusiwa kisheria katika mazingira ambapo wagombea wanakaribiana sana.

Trump alijitangazia ushindi Jumatano na anadai kunya udanganyifu unafanika kumnufaisha Biden.Picha: Tyrone Siu/REUTERS

Ghafla, uongozi wa Warepublican ulipungua kwa chini ya kura 1,000. Wakati zoezi la kuhesabu likiendelea jimboni kote, matumaini ya Gore kushinda yaliongezeka. Majeshi ya mawakili yaliletwa na pande zote - na kufungua malalamiko yao yaliyotokea mahakama kuu ya Florida kwenye mahakama ya juu kabisa nchini Marekani.

Soma pia Trump adai kushinda asipoibiwa na Democratic

AL-Gore mgombea mzuri alieshindwa

Desemba 12, 2000, wiki tano baada ya siku ya uchaguzi, majaji wa mahakama kuu walihukumu kwamba zoezi a kuhesabu kura kwa mkono halikuheshimu viwango vinavyokubaliwa jimboni humo, na kusitisha zoezi la kuhesabu. Na kwa uamuzi huo, mahakama ilimfanya George W. Bush kuwa rais wa Marekani.

Hivyo je, mazingira kama haya yanaweza kujirudia mwaka huu? Ndiyo, anasema Peter Witting, aliyekuwa balozi wa Ujerumani nchini Marekani kuanzia 2014 hadi 2018. Wittig anasema hivi sasa kuna mashauri karibu 400 ya kisheria yanayoendelea katika maeneo tofauti. Haya yote yatawasilisha katika mahakama tofauti, na hivyo tujiandae kwa mapambano ya kisheria.

Je, kinyang'anyiro cha mwaka 2020 kitaamuliwa mahakamani?Picha: Behrouz Mehri/AFP/Getty Images

Lakini Wittig anaiambia DW, kuna tofuati kubwa moja kati ya sasa na wakati ule. Sote tunakumbuka kwamba wakati fulani Al Gore alikubali yaishe na kuondoka kwa maslahi ya taifa. Lakini anasema haamini kama mapambano ya mwana huu yataishia kwa hisia za kimichezo kama ilivyotokea mwaka 2000.

Soma pia Uchaguzi wa Marekani wairarua demokrasia ya kiliberali

Hivi sasa kura zinaendelea kuhesabiwa na taarifa za kina juu ya mapambano yanayotoka ya kisheria bado hazijawekwa wazi - maadamu hakuna kati ya wagombea anakubali kushindwa. Iwapo mapambano ya kisheria yatafika mahakama kuu kama ilivyotokea mwaka 200, Trump anaweza akatulia akijua kuna wingi wa majaji wahafidhina 6 dhidi ya waliberali 3.

Lakini je, mahakama ya juu ya Marekani inaweza kutoa uamuzi wa kisiasa? Hilo pia haliko wazi. Ikiwa hivyo, itakuwa hatua itakayodhoofisha demokrasia ya Marekani na taasisi za serikali zilizojengwa kwa karne kadhaa.

Chanzo: DW