1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je Ulaya ina nafasi gani katika soko la Cobalt ya Congo?

Philipp Sandner John Juma
26 Novemba 2024

Ongezeko la mahitaji ya malighafi muhimu kutengeneza vifaa vya kuwasiliana kielektroniki, limeipa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo fursa mpya ya majadiliano, huku Ulaya ikijitahidi kusambaziwa malighafi hizo.

Katika mji wa Kolwezi, kuna uchimbaji madini wa viwango vyote ukiwemo wa kiviwanda.
Katika mji wa Kolwezi, kuna uchimbaji madini wa viwango vyote ukiwemo wa kiviwanda.Picha: Johannes Meier/streetsfilm

Takriban kilomita 7000 kusini mwa Brussels, karibu na mji wa Kolwezi kunakochimbwa madini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Paul Zagabe Nbanze anafanya kazi katika mgodi wa shaba na cobalt. Hapa, wachimba migodi hufanya kazi kwa mikono yao na kubeba magunia ya kilo 50 ya mawe migongoni mwao.

Sauti zisizokoma za nyundo nzito zikivunja mwamba husikika hapa. Akiwa ameshikilia vipande viwili vya mawe mkononi, Nbanze anasema "tunauza hizi. Wazungu huzinunua, lakini hatujui kwa uhakika wanazitumia kufanya nini

Theluthi mbili ya madini ya cobalt duniani kote, hutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Malengo ya Ulaya ya matumizi ya nishati salama ifikapo 2050

Madini ya Cobalt ni sehemu muhimu ya betri, ambayo ni muhimu kwa mabadiliko ya matumizi ya nishati barani Ulaya. Bara hilo linalenga kufikia matumizi ya nishati salama ifikapo 2050.

Paul Gazabe Nbanze, mchimbaji madini mgodini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoPicha: Johannes Meier/streetsfilm

Huko Brussels Ubelgiji, katika bunge la Umoja wa Ulaya, mjumbe wa Bunge la Ulaya Marie-Pierre Vedrenne, ameelezea msimamo wake kuhusu sera ya umoja huo kuhusu upatikanaji wa malighafi.

Unaweza kusoma pia: Watu waondolewa kwa lazima katika maeneo ya migodi Kongo

Akisisitiza kwamba "Jinsi malighafi zinavyotolewa inapaswa kulingana na maono yetu ya kuepuka unyonyaji, na kuhakikisha watoto hawafanyi kazi katika mazingira ya kutisha."

Ameliambia shirika hili la habari DW kwamba "ni sharti Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya zishirikiane ili kupata usambazaji endelevu na wa kutegemewa, wa malighafi hiyo muhimu"

Cobalt ya Congo yaweza kuwa suluhisho kwa mahitaji ya Ulaya

Kulingana na Cecilia Trasi, mchambuzi wa hali ya hewa na nishati wa taasisi ya Ulaya, Bruegel, Ulaya inahitaji cobalt kutoka Congo ili kuyakidhi mahitaji. "Asilimia 75 ya usindikaji wa cobalt hufanyika nchini China. Kwa hivyo kama unataka kutumia cobalt, ni lazima ufanye biashara na China,"

Marie-Pierre Vedrenne, mjumbe katika bunge la Ulaya asema ipo haja ya kuepuisha unyonyaji wa malighafi ya AfrikaPicha: Johannes Meier/streetsfilm

Vedrenne anafahamu kuhusu ukosefu huo wa usawa na anaeleza kuwa China kwa sasa inadhibiti sekta nyingi za kuongeza thamani zinazohusiana na malighafi. Anasema mbinu za China nchini DRC ni za kinyonyaji, "bila nia ya kujenga uwezo wa kuongeza thamani barani Afrika."

Soma pia: Waasi wa M23 wauteka mji wa madini wa Rubaya nchini Kongo

Wadau wachache wa Ulaya wanapatikana katika baadhi maeneo ya migodi ya DRC. Aidha zipo baadhi ya miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini DRC. Kutokana na juhudi hizo, kuna matokeo chanya japo kiduchu kwani baada ya cobalt kusafishwa nchini China, hupelekwa Ulaya.

China bado inapokea sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya Kongo.

Licha ya juhudi hizo, kuna uwezekano kuwa Ulaya haitakuwa mshirika nambari moja wa kibiashara wa DRC hivi karibuni. China bado inapokea sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya Kongo.

Cecilia Trasi, mchambuzi wa hali ya hewa na nishati wa taasisi ya Ulaya, Bruegel, asema China bado inapokea sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya Kongo.Picha: Johannes Meier/streetsfilm

Soma pia: Rais Felix Tshisekedi asema simu za kiganjani zina damu ya Wakongo

Simon Tuma Waku, mfanyabiashara wa Congo anasema ni jambo la kimantiki kwamba DRC itaepuka nchi za Ulaya kama washirika. Tuma Waku alikuwa waziri wa madini na hidrokaboni wa DRC na alifadhili kanuni ya kwanza ya uchimbaji madini mwaka 2002, baada ya Vita vya Pili vya Kongo.

Kulingana na Waku, mataifa ya Kiafrika yanasema "lazima pia uzingatie matakwa na hisia zetu.

Usitulazimishe kufanya jambo ambalo unaona ni bora kwetu. Badala yake, tuulize tunataka kufanya nini. Na tutakuambia jinsi unavyoweza kuwekeza pesa zako."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW