JE UMOJA WA MATAIFA UTAREJEA IRAQ:
19 Januari 2004Matangazo
NEW YORK: Mkuu wa kiraia wa Kimarekani nchini Iraq,Paul Bremer hii leo anakutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan mjini New York.Wakati wa mkutano huo wakuu hao wanatazamiwa kuzungumzia suala ikiwa na vipi Umoja wa Mataifa utaanzisha tena shughuli zake nchini Iraq.Mkutano huo utahudhuriwa pia na mkuu wa Baraza Tawala la Wairaqi Adnan Pachachi.Umoja wa Mataifa uliondoka Iraq baada ya mashambulio mawili dhidi ya makao yake makuu mjini Baghdad mnamo mwezi Agosti na Septemba kusababisha vifo vya watu 23.Tena siku ya jumapili mshambulizi aliejitolea mhanga aliwaua watu 23 katika shambulio la bomu lililofanywa mbele ya lango la makao makuu ya Marekani na washirika wake mjini Baghdad.Watu wengine 110 walijeruhiwa katika shambulio hilo.Na shambulio jingine la bomu siku hiyo hiyo ya jumapili katika mji wa Kirbala wenye Mashia wengi umewajeruhi watu 13.