Ushawahi kujiuliza hivi ingekuwaje kama ungekuwa bila intaneti? je, upatikanaji wa intaneti ni haki yako ya msingi? Hakuna sheria ya ulimwengu inayosema kuwa ni haki ya msingi. Lakini taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa zinatambua kuwa upatikanaji wa intaneti ni kiwezeshi muhimu cha haki za msingi za kibinaadamu, kama vile uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa taarifa, na hata mikusanyiko.