Wanawake wamekuwa na uwakilishi mdogo katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, hadi sasa. Kabla ya uchaguzi mkuu wa Desemba 20, uungwaji mkono kwa wimbi jipya la wagombea wanawake unaongezeka.
Matangazo
Katika mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mkazi wa eneo hilo Alexandrine Kisikutila anawahimiza watu wote walio karibu naye kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo.Hasa zaidi, kwawagombea wa kike.
"Kama raia wa Kongo niko tayari kupiga kura na kumpigia kura mwanamke," aliiambia DW.
"Sio kwa sababu mimi pia ni mwanamke, lakini kwa sababu ninaamini kuwa wanawake wanaweza kufikia mambo makubwa, kama wanawake kadhaa maarufu duniani walivyothibitisha. Nadhani tunaweza kuendelea kuwa na athari kwa ulimwengu kwa kusaidiana."
Wanawake kwa kawaida wamekuwa hawawakilishwi sana katika siasa za Kongo.Lakini sasa, uungwaji mkono kwa wagombea wa kike unaongezeka - hasa katika maeneo yenye migogoro mashariki mwa nchi.
Kazi yenye 'makuu' na 'isiyo salama'
Wapiga kura nchini Kongo wanatarajiwa kupiga kura Desemba 20 kumchagua rais, pamoja na wawakilishi wa mabunge na mabaraza mbalimbali katika ngazi ya mitaa na kitaifa.
Wapiga kura wataka mabadiliko Kongo
02:54
Lakini kuingia katika siasa haijawahi kuwa rahisi kwa wanawake, ambao bado wanazuiliwa na vikwazo vya kitamaduni.
Generose Kagheni, mratibu wa shirika la Women Today, ambalo linajishughulisha na utetezi wa haki za wanawake katika jimbo la Kivu Kaskazini, anaamini kuwa haki za wanawake mara nyingi zinakiukwa nchini Kongo kwa sababu hakuna wanawake wa kutosha katika nafasi za kufanya maamuzi.
"Uwakilishi mdogo wa wanawake katika vyombo vya kufanya maamuzi ni sababu kuu inayoathiri uzingativu unaotolewa kwa mahitaji yao mahususi, ugawaji wa rasilimali na hata uundaji wa mageuzi ya kisheria, kijamii na kiuchumi," aliiambia DW.
"Ndiyo maana ni muhimu kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki katika ngazi zote za maamuzi ili waweze kuwasilisha na kutetea haki zao katika jamii yetu yenye mfumo dume."
Kama mgombea katika uchaguzi wa urais, Marie-Josee Ifoku anasema anaelewa ni kwa nini wanawake wengi wanakwepa shinikizo lisilokwepeka la kazi ya siasa.
"Ni ulimwengu mkali na usio na usalama," aliiambia DW."Ikiwa huna haiba imara, hautafanikiwa katika siasa."
Ifoku anaongea kutokana na uzoefu.Kama mgombea rasmi wa chama cha Alliance of Elites for a New Congo, alikuwa gavana wa Jimbo la Tshuapa kuanzia 2016-2017 na alikuwa mgombea pekee mwanamke kuwania katika uchaguzi wa urais wa 2018.Lakini licha ya matatizo hayo, ana matumaini kuwa wanawake wengi zaidi watafuata nyayo zake.
"Pamoja na yote, tumeamua kukaidi hofu, kwa sababu lazima ukubali kwamba kuna hofu kubwa nyuma yake, na hiyo inahitaji ujasiri na kuthubutu," alisema.
Kutafuta 'uwezeshaji' na 'maridhiano ya kitaifa'
Kukuza usawa wa kijinsia kote Kongo pengine ni mmoja ya malengo makuu ya wagombea wa kike.
Joelle Bile, mwandishi wa habari na mwanasiasa ambaye anagombea kupitia chama cha Alternative pour un Congo Nouveau (Chama Mbadala kwa Kongo Mpya), alisema wanawake ndio walio katika nafasi nzuri ya kujilinda.
"Kutokana na hadhi yangu kama mwanamke, nadhani ni vigumu kwangu kuachana na ukweli huu muhimu, hivyo niendelee tu kuwaahidi [wapiga kura] kwamba nitakapochaguliwa, nitafanya vizuri zaidi," aliiambia DW.
"Lakini pia, sera zitaundwa ambazo zitahimiza kweli uwezeshaji na maendeleo ya wanawake." Mbali ya usawa wa kijinsia, Bile ana mipango mingine kwa nchi yake akichaguliwa.
"Ningeanza kwa kuomba sensa ya watu. Kuanzia hapo tutapata masuluhisho sahihi ya matatizo ya mara kwa mara ya jamii yetu."
Kuelekea kura hiyo, Ifoku pia anafanya mawazo yake kuhusu mustakabali wa Kongo yajulikane.
"Ninapendekeza kuiondoa jamii ya Kongo katika mfumo wa kizamani kuelekea kitu kipya. Tunatetea uelewa pamoja na maridhiano ya kitaifa," alisema.
Huku uchaguzi ukifanyika katika mazingira ya ghasia zinazoendelea za waasi, sera za utatuzi wa mizozo ni kitovu cha kampeni nyingi.
Machimbo ya madini DRC: Toka jiwe hadi dhahabu halisi
Watu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hutegemea dhahabu kama chanzo kikuu cha kipato. Wachimbaji huhatarisha maisha yao kuchimba mawe ya dhahabu, yanayopitia mikono mingi kabla ya kuwa dhahabu halisi.
Picha: Robert Carrubba
Kazi ya kupasua
Akiwa chini, mchimbaji katika machimbo ya Artisanal hutumia kifaa cha kuchimba mawe ya dhahabu kutoka kwenye udongo. Timu ya uchimbaji huwa na wachimbuaji na wabeba mifuko ya michanga. Wachimbaji hutumia masaa sita hadi nane wakiwa chini ardhini kila siku. Kazi hii huhitaji nguvu. Kwenye machimbo haya, kiasi ya Kilo 200 ya mchanga hutakiwa kuchimbuliwa ili kupata gramu moja ya dhahabu.
Picha: Robert Carrubba
Mifuko kibao ya mawe kwa gramu ya dhahabu
Mchimbaji hupitia njia nyembamba, wakati mwenzake akimsubiri. Mifuko ya mawe ambayo husongamana kuelekea upande wa kuingilia machimboni, huwa iko mbele yake. Ukiachana na kilimo, machimbo ya Artisanal ni muhimu zaidi kwa maisha ya binaadamu katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC.
Picha: Robert Carrubba
Kilo 30 kwa mzigo mmoja
Wabeba magunia ya michanga huipeleka kiwandani kwa ajili ya kusafishwa. Hulipwa Franc za Kongo 500, ambayo ni sawa na Euro 0.29, kwa kiwango cha sasa cha kubadilisha fedha Mashariki mwa Kongo kwa gunia moja na wanaweza kutengeneza kiasi cha pesa kwa siku. Ni miongoni mwa wanaopata kiasi kidogo zaidi cha fedha kwenye machimbo, na katika machimbo haya mara nyingi ni wale walitokea maeneo mengine.
Picha: Robert Carrubba
Kufunikwa kwenye miamba
Mtu huyu amepiga magoti mbele ya mwamba huku akipasua mawe ya dhahabu kwa kutumia jiwe la kupasulia. Baadae mawe yanayobaki huvunjwa kwa njia ya kawaida katikati ya miamba ili kupata dhahabu. Njia hii huchukua muda mrefu; inaweza kuchukua masaa kadhaa kulishughulikia basini moja la plastiki. Wabebaji wa maji na mawe ya dhahabu huonekana wakipanda na kushuka kwenye machimbo.
Picha: Robert Carrubba
Udongo wa thamani
Huyu anamimina udongo wenye dhahabu kwenye mtaro wenye kifaa cha kudhibiti kasi. Madini safi ambayo huletwa na wataalamu wa kifaa hicho huchanganywa na maji na kumwagwa kwenye mtaro wenye udongo. Kutokana na uzito mkubwa, mawe ya dhahabu yanayosalia huganda kwenye blanketi lililokwa mtaroni, wakati masalia humwagikia chini. Mawe hukusanywa na kuchujwa kwenye beseni la plastiki kwa kutumia mekyuri.
Picha: Robert Carrubba
Mauzo ya awali
Mfanyabiashara kutoka machimbo hayo anakagua kiasi gani atakitoa kwa dhahabu aliyoletewa. Dhahabu na madino ya mekyuri yanayoonekana kwenye ndoo ya plastiki ya muuzaji yakiwa na rangi ya chuma na kijivu kabla ya kusafishwa kiwandani. Wachimbaji wengi hutarajia kuuza kiwango kidogo cha dhahabu kwa wafanyabiashara wa eneo la machimbo.
Picha: Robert Carrubba
Kuisafisha dhahabu
Wafanyabiashara wakubwa huunguza dhahabu na acidi ya Nitric kwenye moto mkali ili kuondoa masalia yote. Wafanyabiashara hao hushughulika na kiwango kikubwa sana cha dhahabu kuliko wafanyabiashara wa ndani. Mara nyingi huuza nyingi zaidi kwa wiki. Ziada ya faida yao ni ndogo kuliko wafanyabiashara wa ndani, ingawa huuza kwa kiasi kikubwa, na kujihakikishia kipato kikubwa.
Picha: Robert Carrubba
Poda ya thamani
Baada ya kuichoma, dhahabu inapimwa kwenye mzani wa umeme. Katika hatua hii, dhahabu huwa imefikia kati ya asilimia 92 hadi 98 ya uhalisia wake, kwa kutegemea asili yake.
Picha: Robert Carrubba
Uyeyushwaji wa dhahabu
Baada ya kuyeyushwa, dhahabu huwekwa kwenye chombo cha kutengenezea umbo. Chombo hicho kikishatolewa kwenye moto mkali wa tanuru, mchimbaji kwenye eneo la kuyeyusha humimina dhahabu iliyoyeyuka kwenye kaboni nyeusi ama grafiti kwa ajili ya kutengenezwa umbo. Ndani ya tanuru, dhahabu hufikia kipimo cha joto la digrii 1,500, Celcius. Huchukua takriban dakika 20 kuyeyusha kilo kadhaa za dhahabu.
Picha: Robert Carrubba
Kipindi cha kupoozwa
Dhahabu ambayo tayari imeundwa hutolewa kwenye chombo na kuwekwa na wachimbaji kwenye kwenye eneo la wazi na wakati huo bado hutoa mvuke wa moto.
Picha: Robert Carrubba
tayari kwa kuuzwa!
Ikiwa na kiwango cha dhahabu cha Kilo 4.163 kipisi hiki kina gharama ya takriban Dola 167,056 kwa bei ya soko la London, katika siku iliyozalishwa. Uzalishaji wa dhahabu kwa mwaka Mashariki mwa DRC umekuwa ukikadiriwa kuwa zaidi ya tani 11, lakini dhahabu nyingi inaendelea kuuzwa bei ya ulanguzi nje ya nchi. mwaka 2015, wauzaji rasmi wa dhahabu nje ya nchi walirekodi kiasi cha kilo 254.
Picha: Robert Carrubba
Picha 111 | 11
"Tunataka kuwajenga upya na kuwarejesha Wakongo," alisema Ifoku."Inapaswa kuwa na nguvu, iliojengwa upya na lazima iheshimiwe. Mifagio [inayotumiwa kama nembo ya kampeni] inaashiria mapambano yetu na kujumuisha nguvu. Usafi ni umoja. Ndiyo mpya."