1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washawishi wa mitandaoni wabadili mwelekeo wa Ramadhani?

14 Machi 2024

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, washawishi wa mitandaoni na watengeneza maudhui huko Mashariki ya Kati wanajishughulisha zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko hapo awali.

Mwanamke wa kiislamu ambaye ni mshawishi wa mitandaoni
Mwanamke wa kiislamu ambaye ni mshawishi wa mitandaoniPicha: imago images/Westend61

Harakati hito zimezua hisia mseto, wapo wanaosema watu hao wanaitia doa Ramadhan huku wengine wakisema kuwa wanaweza kuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko yaliyo chanya. Teknolojia imebadilisha namna ambavyo inavyofanyika ibada ya mwezi mzima ya funga ya Waislamu ya Ramadhani. Sasa kuna programu zinazowawezesha wanaodiriki ibada hiyo kufanya kila kitu kuanzia maombi hadi kutoa msaada wao kwa mashirika ya hisani kupitia simu  ya mkononi, hasa ikizingatiwa kuwa jambo muhimu katika  mwezi wa Ramadhan  ni kuwasaidia wenye uwezo mdogo.

Lakini pia kuna maendeleo ambayo yamezua utata zaidi katika ulimwengu wa kidijitali unaohusiana na mwezi wa Ramadhan, na moja wapo bila shaka ni washawishi katika mitandao ya kijamii.

Mwanaume wa Kiislamu akiperuzi kwenye simu yake ya mkononiPicha: Benis Arapovic/Zoonar/picture alliance

Mataifa tajiri ya Ghuba ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi zaidi duniani wenye mawasiliano ya intaneti. Kwa mfano, katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inakadiriwa kuwa asilimia 99 ya watu wanatumia mtandao huo huku nchini Ujerumani ikiwa ni asilimia 93 tu.

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, tafiti zinaonyesha kuwa matumizi ya vyombo vya habari mtandaoni yanaongezeka zaidi kwani watu katika nchi kama vile UAE, Saudi Arabia na Qatar wanatumia muda mwingi zaidi kwenye simu zao na kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo, mwezi wa Ramadhani hupelekea pia ongezeko la manunuzi ya mtandaoni kwa kuwa baada ya  funga ya ramadhan , watu hupeana zawadi na mara nyingi nguo mpya hununuliwa. Katika mwezi huu, kuna desturi ya watu kujumuika zaidi kwenye maombi na milo ya pamoja, watu hupendelea kubadili mavazi mara kwa mara.

Jukumu la Washawishi wakati wa Ramadhani

Wanawake wa Indonesia wakidiriki ibada ya Taraweh katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhan katika msikiti wa Istiqlal mjini JakartaPicha: dapd

Washawishi wa mitandaoni wana jukumu kubwa, na mara nyingi huchukuliwa kama watu wenye wafuasi wengi katika mitando ya kijamii na wanaoweza "kushawishi" maoni na maamuzi ya ununuzi ya wafuasi wao.

Gary Bunt, profesa aliyebobea katika elimu ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Wales na mwandishi wa kitabu kinachofahamika kama "Taratibu za Kiislamu," ameiambia DW kuwa Washawishi hao wanazingatia pia mada za kidini ikiwa ni pamoja na mijadala, mapendekezo kuhusu manunuzi ya bidhaa na michezo gani ya kuigiza inayopaswa kutazamwa katika kipindi hiki.

Soma pia: Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu leo yaanza Ramadhani

Kama ilivyo kwa sekta nyingine, washawishi wa Kiislamu wanaweza pia kuuza bidhaa zao wenyewe au kufadhiliwa ili kuuza bidhaa zingine. Aidha Bunt amesema ongezeko la sasa la shughuli za ushawishi wa mitandaoni huko Mashariki ya Kati umetokana na upanuzi wa majukwaa ya kidijitali, kupunguza mgawanyiko wa kidijitali na hasa ukuaji wa mtandao wa TikTok.

Washawishi katika mataifa ya Ghuba mnamo mwezi huu wa Ramadhani, hujikita zaidi kwenye kutangaza meza zilizopambwa kwa umaridadi zilizotayarishwa kwa ajili ya "iftar," ambao ni mlo wa jioni baada ya funga. Kwa ushirikiano na mashirika ya mitindo ya ndani au yale ya urembo, washawishi hao waliojikita kwenya masuala ya chakula, husaidia kutangaza ofa maalum ya chakula cha Ramadhani au kuitangaza baadhi ya migahawa.

Manunuzi na matangazo kupita kiasi

Mwanaume akifanya manunuzi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan katika duka kubwa la Al-Mubarakiya.huko Kuwait CityPicha: Jaber Abdulkhaleg/AA/picture alliance

Kama ilivyo kwa wakazi wa Ulaya wanavyokosoa sherehe za Krismasi na kuzitaja kuwa ni za kibiashara zaidi, kuna hofu pia katika Mashariki ya Kati kwamba Ramadhani inaelekea pia kuwa ya kibiashara kupita kiasi.

Iyad Barghouthi, mhadhiri wa sosholojia anayeishi katika mji unaokaliwa wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah, ameiambia DW kwamba washawishi zaidi hawajapelekea kuongezeka kwa ibada na badala yake, wamefanya desturi za Ramadhani kuwa zilizopangwa, zisizo na uthabiti wa kiimani.

Marc Owen Jones, profesa msaidizi anayebobea katika masuala ya ubinadamu wa kidijitali katika Chuo Kikuu cha Hamad bin Khalifa cha Qatar, amethibitisha hilo na kusema kuna uhusiano kati ya kuongezeka kwa biashara ya Ramadhani na washawishi na uuzaji wa mitandaoni, jambo linalowakera watu wengi.

Owen ameongeza kuwa  mzozo unaoendelea huko Gaza  unawapa sababu zaidi ya kukerwa na vitendo vya washawishi wanaopigia debe vyakula vya "Iftar" vilivyopindukia kwa wingi huku kukiwa na shinikizo kwa watu kutoshiriki- ama kudhihirisha starehe nyingi za anasa kutokana na kile kinachoendelea huko Gaza.

Vijana wanatuma ibada ya funga kujitafakari

03:06

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW