Je,CIA imevunja sheria kwa kuteketeza kanda za video?
8 Desemba 2007Matangazo
Nchini Marekani,wabunge wa chama cha Demokratik wametoa mwito wa kuchunguza iwapo Shirika la Upelelezi la Marekani CIA lilivunja sheria lilipochukua hatua ya kuteketeza kanda za video zilizoonyesha washukiwa ugaidi wakihojiwa.
Mkuu wa CIA,Michael Hayden amesema,kanda hizo ziliteketezwa mwaka 2005 kwa sababu hazina tena habari za maana za upelelezi na pia zilihatarisha usalama wa mawakala waliohusika.Hayden amekanusha kwamba washukiwa waliteswa kinyume na sheria. Umoja wa Marekani wa Haki za Kiraia na makundi mengine ya haki za binadamu,yamelituhumu shirika la CIA kuwa liliharibu kanda hizo ili kuondosha ushahidi wa vitendo ambavyo huenda ikawa vilihusika na mateso.