1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jenerali Na Man aapishwa Rais wa mpito Guinea Bissau

27 Novemba 2025

Jenerali Horta Nta Na Man ameapishwaAlhamisi 27.11.2025 kuwa Rais wa mpito wa Guinea Bissau baada ya jeshi kutangaza Jumatano kuwa limeipindua serikali ya Rais Umaro Sissoco Embalo.

Jeshi la Guinea-Bissau lilifanya mapinduzi ya kijeshi 26.11.2025
Rais wa mpito wa Guinea Bissau Horta Nta Na ManPicha: Patrick Meinhardt/AFP

Mtawala huyo mpya wa kijeshi ataushikilia wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Mapinduzi nchini humo yamefanyika baada ya uchaguzi mkuu ambapo matokeo yalikuwa bado hayajatangazwa.

Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Mahamoud Ali Youssouf amekilaani kitendo cha jeshi la Guinea Bissau kufanya mapinduzi na kutoa wito wa kuachiliwa huru bila masharti kwa Rais.

ECOWAS yakosoa ukiukwaji wa katiba

Kwa upande wake Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imekosoa vikali mapinduzi hayo na kuyaita ukiukwaji mkubwa wa katiba ya Guinea Bissau. Imetaka pia Embalo na maafisa wengine wanaoshikiliwa na jeshi waachiliwe huru.

Jana Jumatano, milio ya risasi ilisikika karibu na Ikulu ya Rais Umaro Sissoco Embalo, nchini humo siku tatu baada ya uchaguzi wa rais na wabunge.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW