1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Wafungwa 110 waachiwa huru nchini Chad

18 Julai 2023

Kiongozi wa Chad jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, amewasamehe na kuwaachia huru watu wengine 110 zaidi waliokuwa wamepewa vifungo jela, kufuatia maandamano ya kuipinga serikali mwezi Oktoba mwaka jana.

Kiongozi wa Chad jenerali Mahamat Idriss Deby apunga mkono wakati akikaribishwa katika ikulu ya rais ya Elysee nchini Ufaransa tarehe 12 Novemba mwaka 2021
Kiongozi wa Chad jenerali Mahamat Idriss DebyPicha: Michel Euler/AP Photo/picture alliance

Kiongozi wa mashtaka ya umma Mahamat El-Hadj katika mahakama ya rufaa ya N'Djamena, ameliambia AFP kuwa watu hao 110 walikuwa wamepewa vifungo vya kati ya miezi 18 na miaka 5 jela huko Koro Toro, N'Djamena na Moundou, ambao ndio mji wa pili mkubwa nchini Chad.

Watu hao walikuwa wanapinga hatua ya kuuongeza muhula wa mpito Deby.

Jumla ya watu 436 waliokuwa wamehukumiwa vifungo kufuatia maandamano hayo ya Oktoba, wameachiliwa kwa sasa katika kipindi cha chini ya miezi minne. Waandamanaji walikuwa wanapinga hatua ya kuuongeza muhula wa mpito Deby. Deby alitangazwa kuwa rais mnamo mwezi Aprili 2021 baada ya kifo cha babake Idriss Deby Itno aliyekuwa ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 30.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW