1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jengo laporomoka Kariakoo, Dar es Salaam

16 Novemba 2024

Watu kadhaa wahofiwa kufariki baada ya jengo la ngorofa nne kuporomoka katika soko la Kariakoo, Dar es Salaam.

Soko la Kariakoo Dar es Salaam
Operesheni za uokoaji zaendelea baada ya jengo kuporomoka katika soko la Kariakoo.Picha: Yakub Talib/DW

Mtu mmoja ameripotiwa kufa na wengine kujeruhiwa baada ya jengo moja lililolopo eneo la kariakoo Dar es Salam mtaa wa mchikichi  kuanguka.

Inaarifiwa kuwa watu wengine bado wamekwama ndani ya jengo hilo wakiomba msaada kutolewa. Baadhi ya mashuhuda na waokoaji wameeleza DW kuwa kuna dalili kwamba watu baadhi ya watu waliokwama chini ya vifusi vya jengo hilo bado wako hai huku wengine wakisemekana kwamba wanawasiliana kwa simu na watu waliopo nje.

Jeshi la uokoaji Tanzania bado linaendelea na uokoaji,  tunafatilia kwa karibu tukio.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW