1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jepchirchir kutoka Kenya ashinda mbio za marathon Japan

14 Septemba 2025

Mwanariadha Peres Jepchirchir kutoka Kenya ameshinda mbio za marathon kwa wanawake katika mashindano ya riadha ya dunia yaliyofanyika mjini Tokyo Japan. Jepchirchir alimshinda mwanariadha wa Ethiopia Tigist Assefa.

Peres Jepchirchir
Mwanariadha wa Kenya, Peres Jepchirchir ashinda mbio za Marathon JapanPicha: ELSA/Getty Images/AFP

Wanariadha hao wawili walimaliza mbio hizo kwa kuingia katika uwanja wa kitaifa wa Japan bega kwa bega baada ya kukimbia kilomita 42 katika barabara za Tokyo

Assefa alionekana kusonga mbele kabla ya Jepchirchir aliyeshinda medali ya dhahabu katika michezo ya olimpiki mwaka 2021 nchini Japan kuonesha nguvu zake katika dakika za mwisho na kushinda kwa kukimbia kwa saa 2 dakika 24 na sekundu 43

Assifa alichukua nafasi ya pili akiwa nyuma kwa sekunde mbili pekee.

Mwanariadha wa Uruguay Julia Paternain aliweka historia kwa kuchukua medali ya shaba na kuwa mwanariadha wa kwanza kuchukua ushindi wa medali nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW