JERUSALEM. Ariel Sharon amchagua mbadala wa Netanyahu
8 Agosti 2005Waziri wa fedha wa Israel Benjamin Netanyahu mwenye siasa za kihafidhina amejiuzulu wadhfa wake kupinga mpango wa waziri mkuu Ariel Sharon wa kuihama Gaza.
Netanyahu amejiuzulu wakati ambapo serikali ya bwana Ariel Sharon imo katika hatua za mwisho za kuidhinisha kuanza kuhamishwa kundi la kwanza la masetla wa Kiyahudi.
Bwana Benjamin Netanyahu amesha wahi kuwa waziri mkuu wa Israel na vyombo vya habari nchini humo vinagusia uwezekano wa yeye kumpinga Ariel Sharon katika uongozi wa mlengo wa kulia wa chama cha Likud.
Wakati huo huo waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon amemteuwa bwana Ehud Olmert kuchukuwa mahala pa Benjamin Netanyahu.
Kwingineko wanajeshi wa Israel wamemuuwa kwa kumpiga risasi mpalestina mmoja ambaye hakuwa na silaha nje ya nyumba yao.
Walioshuhudia wamesema kuwa wanajeshi walimpiga risasi marehemu mara mbili kichwani na kifuani.