1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Bajeti ya Israel yapitishwa na kamati ya fedha ya bunge

23 Machi 2005

.

Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon amepata ushindi katika kura muhimu leo juu ya bajeti ya nchi hiyo ambayo anatakiwa kuipitisha katika bunge hadi mwishoni mwa mwezi huu ama atakabiliwa na uwezekano wa kufanyika uchaguzi mpya ambao utahatarisha mpango wake wa kujiondoa kutoka katika eneo la Gaza. Kamati ya fedha ya bunge iliidhinisha bajeti hiyo ya mwaka 2005 kwa kura 10 dhidi ya 9 , na kuipeleka bajeti hiyo katika kikao kamili cha bunge ambako Bwana Sharon anakabiliwa na kazi ngumu ili kuidhinishwa kwa bajeti hiyo wiki ijayo dhidi ya Wabunge wenye msimamo mkali wa kizalendo ambao wanapinga dhidi ya kutolewa kwa ardhi yoyote kwa Wapalestina.

Wakati huo huo Israel leo imepiga marufuku Wapalestina kuingia ukingo wa magharibi na Gaza wakati wa sikukuu ya Kiyahudi ya Purim wiki hii, licha ya hatua mpya za amani zilizofikiwa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.