1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Bunge la Knesset lapitisha bajeti ya mwaka huu Israel.

30 Machi 2005

Bunge la Knesset la Israel limepitisha kwa kauli moja bajeti ya mwaka huu jambo ambalo lilikuwa kipingamizi kikubwa kwa waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon katika mpango wake wa kuuhama ukanda wa Gaza.

Uamuzi huu umetokea siku moja baada bunge la Knesset kupinga mswada wa kura ya maoni juu ya mpango wa kuuhama ukanda wa Gaza.

Lakini Masetla wa kiyahudi kupitia shirika linalowawakilisha masettla wamesema kuwa wanapanga kufanya maandamano makubwa kupinga mpango wa Ariel Sharon wa kuihama Gaza.

Mpango huo unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa Julai.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW