JERUSALEM: Bunge launga mkono mpango wa Sharon
13 Januari 2004Matangazo
Bunge la Israel limeunga mkono mpango wa Waziri Mkuu Ariel Sharon kuyatenga kwa kuyagawa maeneo ya Wapalestina. Bunge hilo Knesset limeunga mkono mpango huo kwa kura 51 dhidi ya 39.Iwapo serikali itaamuwa kuendelea na mpango huo Israel itaendeleza ujenzi wa uzio wake katika Ukingo wa Magharibi na kuvunja baadhi ya makaazi ya walowezi ya Kiyahudi.Sharon amesema mpango huo utazidi kuimarisha usalama kwa Waisrael iwapo mpango wa amani unaoungwa mkono kimataifa utashindwa lakini wakati huo huo amesema hatoutelekeza mpango huo unaojulikana kama Ramani ya Amani. Mpango huo unakabiliwa na shutuma kali hususan kutoka ndani ya chama chake mwenyewe cha Likud.Hapo Jumapili zaidi ya watu 100,000 wengi wao wakiwa ni walowezi wamefanya maandamano mjini Tel Aviv kupinga mpango huo.
