1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Condoleezza Rice awasili ukingo wa magharibi.

23 Julai 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili katika eneo la ukingo wa magharibi huko Palestina.

Rice anatarajiwa kukutana na rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas ambako anatarajiwa kumtaka kuhakikisha kuwa kujiondoa kwa Israel kutoka eneo hilo kunatokea bila ya wanaharakati wa wapiganaji wa hamas na Islamic Jihad kufanya ghasia.

Katika hali ya hivi karibu ya ongezeko la ghasia, raia mmoja wa Kipalestina ameuwawa na mwanajeshi mmoja wa Israel amejeruhiwa katika mapigano kati ya wapiganaji hao na jeshi katika mji wa kusini wa ukingo wa magharibi wa Hebron.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW