1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Condoleezza Rice yuko ziarani nchini Israel.

22 Julai 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili nchini Israel kwa ziara ya siku tatu ya mazungumzo yanayotarajiwa kulenga katika mpango wa Israel wa kujiondoa kutoka eneo la ukanda wa Gaza.

Zoezi hilo la kujiondoa , ambalo limepangwa kuanza mwezi ujao , limekumbana na upinzani wa maelfu ya waandamanaji.

Wengi wa walowezi wa Kiyahudi wameapa kutokubali kuziacha nyumba zao katika maeneo yaliyovamiwa ya Wapalestina.

Rice anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon leo Ijumaa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas hapo kesho Jumamosi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW