JERUSALEM Fischer azuru Israel
14 Julai 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani bwana Joschka Fischer, amelilaani shambulio la bomu la kujitoa muhanga lililofanywa katika mji wa Netanya nchini Israel. Wakati wa mkutano wake pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Silvan Shalom, Fischer amesema magaidi ni lazima watengwe mbali na jamii.
Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon amemshukuru Fischer kwa hatua ya Ujerumani kujitolea kikamilifu katika mpango wa kutafuta amani ya mashariki ya kati.
Waziri Fischer ameahidi kwamba Ujerumani na umoja wa Ulaya zinaiunga mkono Israel katika mpango wake wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza. Umoja wa Ulaya unataka kusaidia katika ujenzi wa taasisi nchini Palestina ili kudumisha utulivu huko Gaza.