1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Gaza bado kunatokota

15 Agosti 2006

Jeshi la Israel limesema wanamgambo wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza wamefyatuwa maroketi mawili yaliotengenezwa kienyeji dhidi ya kijiji cha Nahal Oz nchini Israel.

Shambulio hilo linafuatia mashambulizi mawili ya anga ya Israel huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ambapo kwayo watu tisa wamejeruhiwa.Jeshi la Israel limesema lilikuwa likishambulia majengo yenye kuwahifadhi wanamgambo wa Kipelastina.

Pia hapo jana waandishi wawili wa habari kutoka kituo cha Televisheni cha Marekani cha Fox News walitekwa nyara na watu wenye silaha huko Gaza.Hakuna mtu aliyedai kuhusika na utekaji nyara huo.

Msemaji wa serikali ya Palestina inayoongozwa na Hamas imelaani utakeji nyara wa waandishi hao na imetaka waachiliwe mara moja.

Israel ilianzisha mashambulizi huko Gaza baada ya kutekwa nyara kwa mwanajeshi wake mmoja kulikofanywa na wanamgambo wa Kipalestina hapo tarehe 15 mwezi wa Juni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW