JERUSALEM: Israel imeamua kuimarisha mashambulio
9 Agosti 2006Matangazo
Baraza la mawaziri linaloshughulikia masuala ya usalama nchini Israel,limetoa idhini ya kuimarisha mashambulio ya majeshi yake ya ardhi kavu dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon.Lengo ni kuzuia mashambulio ya makombora ya Hezbollah kaskazini mwa Israel.Hapo awali jeshi lilimteua mkuu mpya atakaeongoza operesheni za kijeshi nchini Lebanon.Inasemekana kuwa kamanda huyo mpya,Moshe Kaplinsky ana msimamo mkali zaidi kuliko mtangulizi wake.
