1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel imekataa kusitisha mapigano

30 Julai 2006

Israel imekataa ombi la mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa,Jan Egeland,alietaka mapigano yasitishwe kwa muda wa siku tatu ili misaada iweze kupelekwa kusini mwa Lebanon.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Israel,tayari kuna barabara zinazoruhusu misafara ya kupeleka misaada ya kiutu.Akasema,ikiwa mapigano yatasitishwa,nafasi hiyo huenda ikatumiwa na Hezbollah kujipatia upya silaha na mahitaji mengine.Wakati huo huo misaada imewasili Beirut kwa njia ya ndege na meli kutoka Misri, Jordan,Umoja wa Falme za Kiarabu na Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW