JERUSALEM: Israel imekubali kuchunguza vita vya Lebanon
17 Septemba 2006Matangazo
Serikali ya Israel imeunda kamisheni maalum kuchunguza lawama kuwa katika vita vya Lebanon huenda ikawa kulifanywa makosa.Baadhi kubwa ya mawaziri waliunga mkono pendekezo la waziri mkuu Ehud Olmert kuhusu halmashauri hiyo ya uchunguzi. Madai ya wanajeshi ya kutaka uchunguzi ulio huru, hayakutekelezwa na serikali.Kufuatia mashambulio yaliyofanywa dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah, Olmert alilaumiwa kuwa matayarisho ya kutosha hayakufanywa kabla ya kwenda vitani nchini Lebanon.