1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel imeyafunga maeneo ya Wapalestina

12 Juni 2005

Njia zinazoelekea katika maeneo ya Kipalestina yaliokaliwa na Israel zimefungwa hadi jumatatu,huku Waisraeli wakisherehekea siku kuu ya Kiyahudi ya Shavout.Duru za kijeshi za Israel zimesema,serikali imetoa amri ya kuchukua hatua hiyo kwa sababu ya khofu ya kufanywa mashambulio ya wanamgambo na kuchafua sherehe.Wakati wote wa sherehe hizo,Wapalestina wataruhusiwa tu kuingia Israel kwa sababu za kiutu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW