1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel imeyakabidhi maeneo ya kusini mwa Lebanon

17 Agosti 2006

Jeshi la Israel limesema limeyakabidhi nusu ya maeneo lililoyakalia kusini mwa Lebanon kwa wanajeshi wa Lebanon kufuatia kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Msemaji wa jeshi la kimataifa nchini Lebanon, UNIFIL, amesema kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka eneo hilo kutafanyika katika awamu kadhaa, kwa hiyo itachukua muda kabla wanajeshi wote kuondoka kusini mwa Lebanon.

Ameongeza kusema yote yatategemea uwezo wa jeshi la Umoja wa Mataifa na jeshi la Lebanon kuweza kuyadhibiti maeneo yote ya kusini mwa Lebanon.

Akizungumza kuhusu umuhimu wa kupelekwa kwa majeshi ya kulind amani kusini mwa Lebanon, Malloch Brown wa jeshi la Umoja wa Mataifa amesema, ´Ni mazingira yanayoyumayumba ambapo mtu yeyote anaweza kuchochea na moto wa machafuko ukazuka tena. Tukiweza kuwapokonya silaha wanamgambo kusini mwa mto Litani na kuwapeleka wanajeshi wote wa Umoja wa Mataifa na Lebanon, litakuwa jambo la maana sana.´

Wakati huo huo, Israel inalitaka jeshi la Uturuki kuweka vikwazo katika usafiri wa ardhini na angani, ili kuizuia Iran kuwapelekea wanamgambow a Hezbollah silaha.

Maofisa wa ujasusi nchini Israel wanaamini silaha nzito zilizopelekewa kundi la Hezbollah zilipitia ardhi au anga ya Uturuki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW